MASHARTI YA MATUMIZI – alphatech.co.tz
Karibu kwenye tovuti ya alphatech.co.tz. Kwa kutumia tovuti hii, unakubaliana na masharti ya matumizi yaliyoandikwa hapa chini. Tafadhali yasome kwa makini kabla ya kuendelea kutumia huduma zetu.
1. Kuhusu Alpha Lusubilo Tech
Ni jukwaa la mtandaoni linalowezesha wateja kuagiza bidhaa mbalimbali kutoka China kwa bei nafuu. Tunaratibu uagizaji, tunathibitisha ubora wa bidhaa, na tunahakikisha zinawafikia wateja kwa usalama.
2. Matumizi Halali
Unaruhusiwa kutumia tovuti hii kwa madhumuni halali tu, kama vile kutembelea, kuagiza bidhaa, au kupata taarifa. Hauruhusiwi kutumia tovuti hii kwa shughuli zozote haramu, udanganyifu au uharibifu wa mifumo ya tovuti.
3. Maagizo na Malipo
Bei zote kwenye tovuti ni kwa Tsh (Shilingi ya Tanzania)
Malipo yote lazima yafanywe kwa njia rasmi kama ilivyoelekezwa kwenye tovuti (mfano: TigoPesa, M-Pesa, Airtel Money, Halopesa, au benki).
Oda ya bidhaa huanza kushughulikiwa baada ya kuthibitisha malipo.
4. Muda wa Kufika kwa Bidhaa
Bidhaa huwasili Tanzania kati ya siku 14 hadi 28 kulingana na aina ya bidhaa na usafirishaji. Muda huu ni makadirio na unaweza kubadilika kwa sababu zisizo ndani ya uwezo wetu (mfano: ucheleweshaji wa forodha au usafiri).
5. Sera ya Marejesho
Marejesho au kubadilishiwa bidhaa yatashughulikiwa endapo tu bidhaa imefika ikiwa na tatizo kubwa (mfano: kuvunjika, kutofanya kazi, au siyo bidhaa uliyolipia).
Mteja lazima awasiliane nasi ndani ya siku 3 baada ya kupokea bidhaa ili kudai kurejeshewa au kubadilishiwa.
6. Faragha ya Taarifa
Tunaheshimu faragha ya wateja wetu. Taarifa zako kama jina, namba ya simu, anwani ya usafirishaji, na barua pepe hazitashirikishwa na mtu mwingine bila ruhusa yako, isipokuwa kama ni lazima kwa usafirishaji wa bidhaa zako.
7. Hakimiliki
Maudhui yote kwenye tovuti hii, ikiwemo picha, maelezo ya bidhaa, na nembo ya AlphaTech ni mali ya alphatech.co.tz na hairuhusiwi kunakiliwa bila ruhusa rasmi.
8. Mabadiliko ya Masharti
AlphaTech ina haki ya kufanya mabadiliko ya masharti haya wakati wowote bila kutoa taarifa ya awali. Tunashauri watumiaji kutembelea ukurasa huu mara kwa mara kwa taarifa mpya.
9. Mawasiliano
Kwa maswali au maelezo zaidi, tafadhali wasiliana nasi kupitia:
WhatsApp: +255626101470
📧 Barua pepe: lusubilokayange@gmail.com
0 Reviews